

Lugha Nyingine
(聚焦历史性成就和变革)补齐短板提升效能 公共文化服务着力打通“最后一公里”
Picha hii ikionyesha ndege inayotumia umeme ya kupaa na kutua wima (eVTOL) ikiwa imeegeshwa kwenye eneo la kuchaji katika Bustani ya Luogang mjini Hefei, Mkoani Anhui, mashariki mwa China, tarehe 2 Julai 2025. (Xinhua/Zhou Mu)
LONDON - China inabadilisha muundo wake wa ukuaji kuwa unaozingatia kujitegemea kimkakati, tija inayochochewa na uvumbuzi, na uwezo wa kimfumo, ambao unatoa fursa mpya kwa wawekezaji wa kigeni, amesema Jack Perry, Mwenyekiti wa Klabu ya Kundi la 48 nchini Uingereza.
Kwenye mahojiano ya hivi karibuni na Shirika la Habari la China, Xinhua, Perry amezungumzia ufanisi wa uchumi wa China katika nusu ya kwanza ya mwaka 2025, akirejelea ukuaji thabiti wa Pato la Taifa, pamoja na kupanuka kwa kasi kwa sekta za viwanda vya teknolojia ya hali ya juu na vifaa, uchumi wa kidijitali, na uwekezaji katika utafiti na utengenezaji wa bidhaa.
"China si tu inasawazisha vile inavyozalisha, lakini pia inasawazisha namna na kwa nini inazalisha," Perry amesema.
Roboti ikiandaa kahawa kwenye banda katika Maonyesho ya 26 ya Teknolojia ya Hali ya Juu ya China (CHTF) mjini Shenzhen, Mkoani Guangdong, kusini mwa China, Novemba 14, 2024. (Xinhua/Mao Siqian)
Akiwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mauzo ya Nje la London, Perry amesema mahitaji ya kimataifa kwa uvumbuzi wa China yanayongezeka siku hadi siku.
"Kampuni za Mashariki ya Kati, Ulaya, na Amerika Kusini zinatafuta teknolojia za hali ya juu, za kisasa kutoka China, si kwa sababu ni nafuu, lakini kwa sababu ni bora zaidi." amesema.
Watembeleaji maonyesho wakitazama gari la kampuni ya Xiaomi SU7 kwenye Kituo cha Maonyesho cha Zhongguancun mjini Beijing, mji mkuu wa China, Juni 20, 2025. (Xinhua/Ju Huanzong)
Katika wakati wa kuongezeka kwa kujilinda kibiashara na mgawanyiko wa kibiashara duniani kote, Perry amepongeza dhamira ya China ya kuendelea kufungua mlango.
"Wakati nchi nyingi zinageukia ndani na kujenga kuta, China inafanya kinyume chake. Inapanua uhusiano wake wa kiwenzi, kuzidisha kwa kina uhusiano wa kibiashara, na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa," amesema.
Amerejelea mapendekezo kama vile maendeleo ya Ukanda Mmoja, Njia Moja na makubaliano mapya ya biashara kama ushahidi wa mkakati wa kivitendo wa China.
Kwa mujibu wa Perry, kampuni za kimataifa zinaendelea kuwa na matumaini kuhusu China.
"Baadhi ya kampuni zenye mtazamo wa siku za baadaye zaidi duniani zinasogea karibu na China, si kwenda mbali. Zinatambua kiwango, uwezo, na mazingira ya uvumbuzi kama muhimu kwa uwezo wao wenyewe wa ushindani." amesema.
Ametaja sekta kadhaa ambazo zinatoa fursa muhimu kwa wawekezaji wa kigeni, zikiwemo za mifumo ya kufuata AI, miundombinu ya nishati, huduma za kuuza nje roboti, mifumo ya kisasa ya usafiri, na majukwaa yanayoaminika ya bidhaa.
Jack Perry, mwenyekiti wa Klabu ya Kundi la 48, akitoa hotuba kwenye mkutano wa 2025 wa "Wekeza Nchini China" mjini London, Uingereza, Aprili 4, 2025. (Xinhua/Jia Yuchen)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma